Wanafunzi 8 nchini Kenya washikiliwa na polisi kufuatia ajali ya moto katika shule ya wasichana

Mbali na mauaji yaliyotokea, moto huo uliowaka usiku wa kuamikia Alhamisi pia ulijeruhi wengine 79.

Newstimehub

Newstimehub

29 Mei, 2026

d7580d9ca007001d0e0caa8c7a63bf1f53653b1baf4dda7830582413c44b6178

Polisi nchin Kenya wamewakamata wanafunzi wanane wakike wanaoshukiwa kuchoma moto uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 na wengine kujeruhiwa katika shule ya wasichana ya Utumishi Girls School katikati mwa nchi hiyo.

Mamlaka zimesema bado haijafahamika chanzo cha kufanya hivyo wakati uchunguzi ukiendelea.

Wasichana hao wamekamatwa kwa kupanga na kutekeleza tukio la uchomaji moto katika shule hiyo ya wasichana ya Utumishi, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.

Mbali na mauaji yaliyotokea, moto huo uliowaka usiku wa kuamikia Alhamisi pia ulijeruhi wengine 79.

Ukamataji huo umefanyika baada ya polisi kutumia siku nzima kuwahoji wanafunzi bila wazazi wao.

“Wachunguzi wamefanya mahojiano ya kina na wanafunzi, walimu, na mashuhuda wengine, huku vikosi vya vikiendelea na tathmini ya picha za CCTVT,” amesema John Matere, ambae ni msemaji wa DCI.

Mpaka sasa, wazazi bado hawana taarifa kamili ya lini watoto wao waliokamatwa wataachiliwa.

“Hata hatujaambiwa kuhusu wanafunzi wanane waliokamatwa,” amesema mmoja wa wazazi, ambae hakutaka jina lake litajwe kwa kuhofia binti yake anaweza kuadhibiwa, ameiambia AP.

“Tuko hapa na hakuna anayetupa taarifa yoyote.”

Mpaka sasa, sababu ya kuchomwa kwa bweni la shule hiyo haijafahamika.

“Wachunguzi wanaendelea kuchukua taarifa na kutathmini ushahidi uliopo, ili kubaini chanzo cha kufanya hivyo,” amesema Matere katika taarifa yake.

Miili ya wanafunzi 16 waliofariki imepelekwa katika mochwari ya hospitali ya serikali Alhamisi, ili kupimwa vinasaba na kuwatambua.

Ajali za moto mashuleni zimekuwa zikitokewa mara kwa mara Afrika Mashariki, hivyo kuibua hali ya wasiwasi kuhusu usalama wa watoto.

Mara kadhaa chanzo kimekuwa hitilafu ya umeme.