Mfalme Oyo Nyimba: Mwili wa mfalme mdogo zaidi warudishwa Uganda kwa mazishi

Mwili wa mfalme Oyo Nyimba uliwasili kwa ndege katika uwanja mkubwa wa nchi hiyo ambapo Rais Yoweri Museveni alikuwa miongoni mwa waliofika kuulaki.

Newstimehub

Newstimehub

4 Septemba, 2026

235e0450 dd4f 4b02 b35f bf2d57137ae8 1788535093667

Mwili wa Mfalme Oyo Nyimba, ambaye alikuwa mfalme mwenye umri mdogo zaidi duniani alipochukua hatamu akiwa miaka mitatu mwaka 1995, umewasili nchini Uganda siku ya Ijumaa baada ya kufariki dunia kutokana na saratani, na kabla ya mazishi yake Septemba 12.

Mfalme Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV wa Ufalme wa Tooro. moja ya falme nyingi za kijadi nchini humo na ulioko karibu na milima ya Rwenzori magharibi wa Uganda, alifariki dunia Agosti 27 nchini Marekani alikokuwa anatibiwa.

Alikuwa na umri wa miaka 34.

Kikatiba Uganda ni jamhuri na mamlaka kamili anayo mkuu wa nchi aliyechaguliwa na wananchi. Lakini falme za nchi hiyo zilokuwepo tangu kale kabla ya ukoloni bado zipo na zina ushawishi mkubwa kitamaduni na kijamii.

Kuna video inayomuonesha akichukua hatamu za uongozi 1995 akiwa amekaa kwenye kiti, huku mwili wake mdogo ukizama ndani ya taji na joho kubwa alilovalishwa. Kuchukua uongozi akiwa na umri mdogo kama huo kulimfanya apendwe na wengi.

Museveni katika uwanja wa ndege

Mwili wa Oyo Nyimba uliwasili kwa ndege ya kukodi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe ambapo Rais Yoweri Museveni alikuwa miongoni mwa watu wachache waliofika kuulaki.

“Hatuamini kweli kama mheshimiwa hayupo tena nasi, (ni kama) bado tuko kwenye ndoto na naomba kama ingekuwa ndoto kweli,” alisema mbunge Jennifer Mujungu, ambaye eneo bunge lake liko sehemu ya ufalme wa Oyo Nyimba.