Japan yamnyonga mtu aliyeua watu 5

Takami alikutwa na hatia ya kuchoma moto jengo moja nchini humo, tukio lililotokea Julai 5, 2009.

Newstimehub

Newstimehub

21 Agosti, 2026

4714db72 5a10 46e6 b2fe a16fa4bd2bba 1787311778532

Serikali ya Japan imetoa adhabu ya kifo kwa mtu mmoja, aliyehusika na vifo vya watu watano.

Hii inakuwa adhabu ya kwanza ya kunyonga mtu, tangu Sanae Takaichi achaguliwe kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Oktoba mwaka jana.

Mahakama ya nchi hiyo, ilitoa hukumu hiyo mwaka 2016 kwa Sunao Takami, mwenye umri wa miaka 58, kabla ya kuitekeleza siku ya Ijumaa.

Takami alikutwa na hatia ya kuchoma moto jengo moja nchini humo, tukio lililotokea Julai 5, 2009.

Watu wapatao 10, walijeruhiwa katika tukio hilo.

“Nilitoa uamuzi wa kumnyonga mtu huyo, mara baada ya kujiridhisha na ushahidi wote,” alisema Waziri wa Sheria wa Japan, Hiroshi Hiraguchi mara baada ya hukumu hiyo kutekelezwa siku ya Ijumaa.