Ufaransa yapitisha sheria ya ‘kusaidia watu kufa’

Chini ya sheria hiyo, wagonjwa watakuwa na haki ya kupewa dawa maalumu ambayo itaongeza kasi ya kifo kwa mgonjwa husika, ili kumuondolea mateso.

Newstimehub

Newstimehub

19 Agosti, 2026

2a4f2218 65ef 4243 884c c524173b0903 1787128031266

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, ameidhinisha sheria mpya inayotoa haki ya kusaidia watu, hususani wagonjwa walioko kwenye hali mbaya, kufikia mwisho wao wa maisha.

Uamuzi wa kupitisha sheria hiyo, unakuja baada ya miaka mingi ya kujadiliwa bungeni.

Kwa sasa, sheria hiyo ipo kwenye gazeti ramsi la serikali ya Ufaransa, baada ya kupitishwa na Baraza la Katiba, wiki iliyopita.

Chini ya sheria hiyo, wagonjwa watakuwa na haki ya kupewa dawa maalumu ambayo itaongeza kasi ya kifo kwa mgonjwa husika, ili kumuondolea mateso.

Dawa hizo, zitatolewa na wataalamu wa afya, kulingana na sheria hiyo.

Kulingana na sheria hiyo, ni lazima mgonjwa anayekusudiwa kupewa dawa hizo awe raia wa Ufaransa, awe na hadhi ya ukaazi wa muda mrefu nchini humo na awe na ugonjwa usioweza kutibika.