Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema kuwa Urusi inajipanga kuandaa makombora ya kutosha kutoka Korea Kaskazini, ili iishambulie nchi yake.
Kwa mara kadhaa sasa, Zelensky ametadhaharisha kuhusu ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Korea Kaskazini.
“Kwa mara ya kwanza, Urusi wanashindwa kuingia vitani, bila kutumia msaada wa kivita kutoka Korea Kaskazini,” alisema Zelensky siku ya Jumatatu.
Hata hivyo, kiongozi huyo hakutoa ushahidi wowote wa muda wenye kuonesha hayo anayodai kufanyika.
Hata hivyo, alizitaka Japan na Korea Kusini, kuisaidia nchi kivita, ili iweze kukabiliana na na vitisho vya Urusi, ambavyo vimeongezewa nguvu na Korea Kaskazini.
Juma lililopita, Zelensky alidai kuwa, jumla ya wapiganaji 50,000 wa Korea Kaskazini, walikuwa wamewasili nchini Urusi.
Korea Kaskazini ni mshirika wa karibu wa kijeshi wa Urusi, toka Rais Vladimir Putin na Kim Jong Un, watiliane saini mkataba wa kusaidiana kijeshi, Juni mwaka 2024.















