Venezuela yaiwekea soko huria sekta yake ya mafuta

Hatua hiyo, inakuja takribani wiki tatu, tangu Marekani imuondoe madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro, ambaye mtangulizi wake Hugo Chavez alilazimisha utaifishwaji wa makampuni ya nje ya mafuta katikati ya miaka 2000.

Newstimehub

Newstimehub

22 Januari, 2026

1769111363370 v3z9wx 50bfb9fdca0479e25313fc3be8e2d5425d5c1820fe405c7ab19dddc8599e9891

Wabunge wa Venezuela wameanza mkakati wa kuisogezea sekta binafsi ya taifa hilo, fursa zinazopatikana kwenye sekta ya mafuta ya nchi hiyo.

Hatua hiyo, pia inatajwa kuwa kama habari njema kwa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ameonesha kushawishika na fursa hiyo.

Muswada wa watunga sheria hao, unahitimisha miongo umiliki wa serikali kwenye sekta hiyo.

Hatua hiyo, inakuja takribani wiki tatu, tangu Marekani imuondoe madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro, ambaye mtangulizi wake Hugo Chavez alilazimisha utaifishwaji wa makampuni ya nje ya mafuta katikati ya miaka 2000.

Muswada huo, pia umepigiwa chapuo na makamu wa zamani wa Maduro, Delcy Rodriguez.

Wakati huo huo, Marekani imemteua Laura F. Dogu, kama mwakilishi wake mpya nchini Venezuela.

Hatua hiyo, inatajwa kama mwanzo wa kurejesha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.