Mchakato wa kuirudisha Uturuki kwenye mradi F-35 ni wakiridhisha, asema Seneta Turner

Kulingana na Turner, wawakilisha waliohudhuria mazungumzo hayo, wameonesha matumaini ya hatua zinazoendelea, japo hakuwa tayari kuweka wazi kilichojadiliwa kati ya maofisa wa Uturuki na wabunge wa Marekani.

Newstimehub

Newstimehub

16 Julai, 2026

f57063cc f60a 4ce7 8d3a 312e73a7a5e4 1784209839070

Seneta wa Marekani, Mike Turner amesema kuwa mazungumzo ya kuirejesha Uturuki katika mradi wa ndege za kivita za F-35 ni wa kuridhisha.

Kulingana na Turner, wawakilisha waliohudhuria mazungumzo hayo, wameonesha matumaini ya hatua zinazoendelea, japo hakuwa tayari kuweka wazi kilichojadiliwa kati ya maofisa wa Uturuki na wabunge wa Marekani.

“Kwa pamoja, tunaweza kusema kuwa maendeleo yanaridhisha,” alieleza Turner, akibainisha kuwa hayo yalikuwa ni mawazo sawa na Seneta Jeanne Shaheen, wa Democrat.

Turner alielezea urejeshwaji wa Uturuki katika mradi huo, kama jambo lenye umuhimu mkubwa.

 “Ni wanachama wa NATO, wanachama wenye ushawishi mkubwa, hususani kwa kuwa wenyeji wa mkutano wa NATO ambao ulikuwa wa mafanikio makubwa,” alisema.

Turner, aligusia nafasi ya awali ya Uturuki katika uzalishaji wa ndege hizo za kivita za kizazi cha tano.