Rais Mnangagwa apitisha sheria ya kumuongezea muda wa kukaa madarakani

Hata hivyo, sheria hiyo ambayo inaondoa uchaguzi wa urais, imepingwa na vyama vya upinzani vya nchini Zimbabwe.

Newstimehub

Newstimehub

7 Julai, 2026

51524b3406d3beff4f91e123a4f745e0b4457573bf697764d1fd922b5ab623f8

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, ametia saini sheria inayomuongezea muda madarakani, hadi mwaka 2030.

Hata hivyo, sheria hiyo ambayo inaondoa uchaguzi wa urais, imepingwa na vyama vya upinzani vya nchini Zimbabwe.

“Sasa ni rasmi, imekuwa sheria,” alisema Afisa Mwandamizi ndani Wizara ya Habari wa nchi hiyo Nick Mangwana, kupitia ukurasa wa X.