Senegal imekata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kupinga uamuzi wa kunyang’anywa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika na kukabidhiwa kombe hilo Morocco.
Mahakama hiyo yenye makao yake Uswizi ilithibitisha siku ya Jumatano kwamba Senegal imewasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo.
“Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) inathibitisha kupokea rufaa kutoka Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) dhidi ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Morocco,” CAS iliandika katika taarifa.
Senegal wanataraji kubatilisha uamuzi wa shirikisho la soka barani Afrika wa kuwanyang’anya taji hilo baada ya baadhi ya wachezaji wao kutoka nje ya uwanja wakipinga penalti iliyotolewa kwa Morocco wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika tarehe 18 Januari, mchezo ambao Senegal walishinda 1-0 katika muda wa nyongeza.
Chanzo: Newstimetr














