Mahakama ya Kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imewahukumu kunyongwa, wanajeshi 66 kwa makosa mbalimbali, ikiwemo uasi na kutotii maagizo kutoka kwa wakubwa wao.
Hukumu hiyo, iliyotolewa na Mahakama ya Kijeshi ya Goma, kaskazini mwa Kivu, ilihusisha wanajeshi 70, huku wanne kati yao wakiachiwa huru, na mwingine mmoja kupewa kifungo cha mwaka mmoja jela.
Wanajeshi hao, ni sehemu ya kikosi cha 3415 cha jeshi la DRC, ambao walikamatwa Oktoba 20, katika eneo la Walikale.
Kulingana na jeshi la nchi hiyo, uamuzi huo unalenga kuimarisha nidhamu ndani ya majeshi ya ulinzi ya DRC, wakati wa operesheni ya kurejesha amani, katika eneo la mashariki la nchi hiyo.
Mwezi uliopita, mahakama ya kijeshi ya DRC, iliwahukumu kunyongwa, wanajeshi 27 kwa kuonesha uoga, kufuatia uamuzi wao wa kujiondoa kwenye uwanja wa mapambano, wakati wa vita dhidi ya vikundi vya waasi wa AFC/M23.















