Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki Burhanettin Duran ametoa wito kwa serikali, wanahabari, wasomi na mashirika ya kiraia katika dunia ya Kiislamu kushirikiana kuimarisha uwezo wa habari na teknolojia ya kidijitali.
Duran alisema ili jamii za Kiislamu ziweze kushindana katika zama mpya za uundaji wa simulizi, ni lazima ziwekeze zaidi katika elimu ya kidijitali, taasisi za kupambana na upotoshaji wa taarifa na majukwaa ya kujieleza kimataifa.
Alisisitiza kuwa mazingira ya sasa ya kimataifa yanatoa nafasi kwa ulimwengu wa Kiislamu kujenga upya taswira yake na kushiriki kikamilifu katika kuunda mfumo mpya wa dunia.
Kwa mujibu wake, bila juhudi hizo, sauti za jamii za Kiislamu zitaendelea kutawaliwa na simulizi zinazoundwa na wengine nje ya ulimwengu wa Kiislamu.
CHANZO: Newstimetr














