Hatua mpya ya Uturuki katika kusimamia mitandao ya kijamii na michezo ya mtandaoni inalenga kupunguza hatari ambazo watoto na vijana hukumbana nazo wanapotumia majukwaa ya kidijitali.
Kanuni hizo mpya zinatoa msisitizo mkubwa kwa usimamizi wa wazazi, uthibitisho wa umri, na uwajibikaji wa kampuni za mitandao katika kuondoa maudhui hatari kwa wakati.
Mamlaka zinasema kuwa mfumo huu utawafanya watoa huduma kuwajibika zaidi, hasa pale ambapo maudhui yaliyopigwa marufuku yanaweza kurudi tena mtandaoni. Ndiyo maana matumizi ya akili mnemba yameingizwa kama sehemu ya ufuatiliaji wa mara kwa mara.
Kwa upande wa michezo ya mtandaoni, sheria hizo zinakataza michezo isiyo na udhibiti wa umri na kuweka masharti kwa kampuni za kigeni zilizo na watumiaji wengi nchini Uturuki kuwa na mwakilishi wa kisheria.
Serikali inaamini kuwa sheria hizi zitasaidia kujenga mazingira salama, ya uwazi na yenye ulinzi zaidi kwa watoto na vijana. Utekelezaji wake unaanza rasmi miezi sita baada ya kutangazwa.
CHANZO: Newstimetr














