Wasanii na wachambuzi wa muziki barani Afrika wamesema urithi wa Papa Wemba bado unaendelea kuathiri kizazi kipya cha wanamuziki hata miaka 10 baada ya kifo chake.
Mbali na muziki, Papa Wemba anakumbukwa kwa kueneza utamaduni wa La Sape, mtindo wa maisha unaohusisha mavazi ya kifahari, kujiamini na utambulisho wa kisanii.
Wadau wa muziki wanasema mchango wake umeonekana katika maendeleo ya Afrobeat ya kisasa, rumba ya Congo na namna wasanii wa Afrika wanavyojenga taswira zao jukwaani.
Kwa wengi, Papa Wemba hakuwahi kuwa tu msanii wa muziki, bali alikuwa alama ya utamaduni wa Kiafrika inayozidi kuishi kupitia kizazi kipya cha wasanii.
CHANZO: Newstimetr














