Ugonjwa wa Ebola wasitisha mkutano kati ya Umoja wa Afrika na India

Ujazo wa biashara kati ya India na Afrika ulifikia Dola bilioni 93.69 kwenye mwaka wa fedha 2025-26.

Newstimehub

Newstimehub

21 Mei, 2026

1779380805461 qo4h9m be7713d338c887f1a412cb819eec01f32dd3fbd5f2ef3ab978726189edf9cd64

Mkutano kati ya Umoja wa Afrika (AU) na India, uliokuwa ufanyike mwezi huu, umeahirishwa kutokana na ugonjwa wa Ebola ambao umekumba nchi kadhaa za Afrika.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya India siku ya Alhamisi, ilisema kuwa mkutano huo sasa utafanyika wakati mwingine.

Kulingana na serikali ya India, pande hizo mbili zilifanya tathimini ya pamoja ya hali halisi inavyoendelea katika maeneo mbalimbali barani Afrika, na kuona umuhimu wa kuahirisha mkutano huo.

Awali, mkutano huo ulipangwa kufanyika kuanzia Mei 28 hadi 31 jijini New Delhi.

Tarehe mpya za mkutano huo, zinatarajiwa kuwekwa wazi mara baada ya wajumbe kutoka pande hizo kukutana.

Ujazo wa biashara kati ya India na Afrika ulifikia Dola bilioni 93.69 kwenye mwaka wa fedha 2025-26.