Tunisia kutoza faini wanaosambaza ‘taarifa za kupotosha’ badala ya kifungo kwa uhalifu wa mitandaoni

Marekebisho kwa sheria ya uhalifu wa mitandaoni imeweka faini ya hadi $6,600, huku wale wanaorudia makosa bado wanaweza kuhukumiwa kifungo gerezani

Newstimehub

Newstimehub

1 Oktoba, 2026

5a4c0f87 7ac3 44c8 a8a8 5b72b2a1db24 1790838094347

Tunisia itaanza kutoza faini badala ya kuwafunga jela wale wanaosambaza “taarifa za kupotosha” chini ya sheria yake ya uhalifu wa mitandaoni, kulingana na marekebisho kwenye Gazeti Rasmi la serikali siku ya Jumatano.

Kablaba ya mabadiliko hayo, kifungu 54 kilikuwa kinapendekeza kifungo cha hadi miaka mitano gerezani kwa kusambaza taarifa za uwongo ambazo huenda zikawa hatari kwa usalama au kuwa kikwazo kwa haki za wengine.

Chini ya kifungu kilichofanyiwa marekebisho, makosa kama hayo sasa watatozwa faini ya kati ya dinari 10,000 na 20,000 za Tunisia ($3,300-$6,600).

Adhabu kama hiyo pia iko kwa wale wanaosambaza nyaraka za uongo au kupotosha, taarifa binafsi za watu au madai ya uongo kuwaharibia watu sifa, heshima yao, kuharibu utu, kuchochea mashambulizi au matamshi ya uchochezi.

Watakaorudia makosa bado wanaweza kufungwa gerezani hadi miezi sita pamoja na faini ya dinari 50,000 (zaidi ya $16,000), huku adhabu zikiwa maradufu pale mtu anapokuwa mtumishi wa umma au mtu aliye katika nafasi kama yake.

Marekebisho hayo yanakuja baada ya mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumanne yaliyoongozwa na Rais Kais Saied kuangazia mabadiliko ya kifungu cha 54 na sheria zingine.

Kifungu hichi cha kimekosolewa na mashirika ya haki za binadamu kuhusu athari zake kwa uhuru wa kujieleza.