Erdogan aupongeza mkutano wa COP31, auita wenye mafanikio makubwa kihistoria

Erdogan ametoa kauli hiyo wakati akihutubua mkutano wa vijana wa chama cha AK, uliofanyika jiini Ankara siku ya Jumatatu.

Newstimehub

Newstimehub

16 Novemba, 2026

cb4f1a65 4bd5 4cef 9125 3cce29909ab5 1794837144131

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, amepongeza Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) uliondaliwa na Uturuki, akiulezea kuwa wa mafanikio kihistoria katika maandalizi na mahudhurio yake.

Erdogan ametoa kauli hiyo wakati akihutubua mkutano wa vijana wa chama cha AK, uliofanyika jiini Ankara siku ya Jumatatu.

Akizungumzia mkutano mwingine wa NATO uliofanyika jijini Ankara mwezi Julai, Erdogan alisema mkutano huo unaendelea kuwa na faida hadi kufikia sasa.

“Bado tunaendelea kuona faida za mkutano huo. Faida zake zinaonekana ulimwenguni mzima,” alisema.

Akigusia ushawishi wa Uturuki ambao unaendelea kuongezeka, Erdogan alisema kuwa nchi hiyo itaendelea kutilia mkazo suala la elimu duniani, huku miradi ya ndani ikiendelea kuvutia macho na masikio duniani.

“Kadiri mfumo mpya wa dunia unavyojitokeza, ni nyinyi ambao mtaifanya Uturuki kuwa kitovu cha kila uhalisia,” alisema Erdogan  wakati akiwahutubia vijana hao.