Thailand imeweka masharti ya kukaa karantini 21 kwa wasafiri wanaotoka au waliopitia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo au Uganda, ambapo maambukizi ya Ebola yanaongezeka.
Kuna mlipuko wa Ebola mashariki mwa DRC kiasi cha Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza hali ya tahadhari.
Tangu DRC kutangaza mlipuko huo Mei 15, ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu 204 na maambukizi yanayoshukiwa kuwa 867, kulingana na taarifa iliotolewa na wizara ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa wiki.
Katika nchi jirani ya Uganda, mtu mmoja amefariki, huku wengine sita wakithibitishwa kuambukizwa.
Inaambukiza haraka
Wasafiri walio na dalili au wasio “na dalili za Ebola lazima wakae karantini kwa siku zisizopungua 21”, wizara ya afya ya Thailand imesema katika taarifa siku ya Jumanne.
Thailand haijakuwa na maambukizi yoyote ya wasafiri kuwa na virusi vya Ebola lakini kuna hatari kutokana na watu kusafiri duniani, afisa mwandamizi wa wizara ya afya Somlerk Jeungsmarn amesema katika taarifa.
Wale wenye dalili za Ebola lazima wakae karantini katika hospitali ya serikali iliotengwa mahsusi kwa ajili hiyo, ilhali wale ambao hawatokuwa na dalili watahitajika kukaa maeneo fulani, wizara ilisema.
















