Maafisa wa serikali nchini Nigeria wametetea shambulizi la anga lililofanyika katika eneo la kaskazini mashariki, wakisema lililenga wapiganaji wa Boko Haram.
Gavana wa jimbo la Borno State, Babagana Umara Zulum, alisema soko lililoripotiwa kushambuliwa lilikuwa limefungwa rasmi miaka mitano iliyopita kwa sababu lilikuwa linatumiwa na magaidi kama kituo cha usambazaji wa vifaa.
Jeshi lilieleza kuwa mashambulizi hayo yalikuwa sehemu ya juhudi za kuwasaka magaidi waliokuwa wakikimbia na kujipanga upya katika eneo hilo lenye mazingira magumu.
Nigeria imekuwa ikikabiliana na uasi wa Boko Haram kwa zaidi ya muongo mmoja, hali ambayo imesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.
CHANZO: Newstimetr














