Mlipuko wa Ebola ‘unasambaa kwa kasi’ DRC huku watu zaidi ya 2,500 wakifariki: UN

Mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sasa umesambaa katika eneo lililo kubwa zaidi ya taifa la Ufaransa, anasema mratibu mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa.

Newstimehub

Newstimehub

21 Agosti, 2026

3b35d1f4 9e64 4c18 9d7d eb05c81b3c5b 1787335594145

Mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia unasambaa “kwa kasi,” huku watu zaidi ya 2,500 wakifariki katika kipindi cha miezi mitatu iliopita, mratibu mwandamizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ugonjwa huo alisema siku ya Ijumaa.

“Ugonjwa huo unasambaa kwa kasi. Sasa umesambaa katika eneo lililo kubwa zaidi ya taifa la Ufaransa,” Julien Harneis aliwaambia waandishi wa habari.

“Unasambaa kwa haraka na unazidi mikakati ya kukabiliana na Ebola,” alisema.

Harneis alieleza kuwa nusu ya vifo hivyo vimetokea katika kipindi cha siku 20 ilizopita.

Harneis anasema mapigano nchini DRC, ambayo yameendelea kwa njia mbalimbali tangu 1999, yamesababisha watu zaidi ya milioni 1 kuondoka katika makazi yao kwenye maeneo yaliyoathirika, huku yakitatiza shughuli za maafisa wa usalama na utoaji wa huduma za msingi, hasa za afya.

Pia alieleza kuhusu hali ngumu kwa wafanyakazi wa afya wanaokabiliana na mlipuko huo, ambapo zaidi ya 5,000 wameambukizwa tangu mwezi Mei.

“Wahudumu wa afya 160 wameambukizwa Ebola, na 43 wamefariki,” Harneis alisema.