Mashambulizi ya risasi yawauwa watu 17 Afrika Kusini

Polisi wamesema kuwa tukio hilo linadaiwa kutokea kati ya saa nne usiku na saa tano usiku wa 15 Novemba 2026.

Newstimehub

Newstimehub

17 Novemba, 2026

65b6c05c a23f 485f b63e 8174521d4408 1794907609390

Polisi nchini Afrika Kusini bado hawajabaini chanzo cha matukio mawili ya ufyatuaji risasi wa halaiki yaliyotokea tarehe 15 Novemba 2026 na kusababisha vifo vya watu 17.

Matukio hayo yalitokea katika maeneo tofauti yenye umbali wa takriban kilomita 530.

Watu wanane walikutwa wakiwa wamefariki dunia ndani ya gari lililotobolewa kwa risasi katika eneo la Sweetwaters, nje ya mji wa Pietermaritzburg.

Wengine tisa walikutwa wamefariki dunia wakiwa na majeraha ya risasi katika makazi yasiyo rasmi ya eneo la Jeffsville, karibu na mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria.

Tukio la Jeffsville linachunguzwa na kitengo kinachoshughulikia uhalifu mkubwa na wa kikatili, mauaji, na uporaji katika jimbo la Gauteng.

Polisi wamesema kuwa tukio hilo linadaiwa kutokea kati ya saa nne usiku na saa tano usiku.

“Polisi walitaarifiwa majira ya saa moja unusu za asubuhi ya leo, tarehe 16 Novemba 2026. Walipofika eneo la tukio, walikuta miili ya watu tisa—wanaume sita na wanawake watatu—ndani ya kibanda chenye vyumba vinne, wakiwa na majeraha ya risasi,” alisema msemaji wa polisi, Brenda Muridili.

Polisi walisema kuwa sababu za mashambulizi hayo bado hazijabainika mara moja.

Tukio hilo linachunguzwa na kitengo kinachoshughulikia uhalifu mkubwa wa kikatili, mauaji, na uporaji katika jimbo la Gauteng.

Kamishna wa Polisi wa Gauteng, Tommy Mthombeni, alisema mauaji hayo yanaweza kuhusishwa na tukio la ufyatuaji risasi katika makazi yasiyo rasmi yaliyo karibu, huko Saulsville, mwaka jana, ambapo watu 12 waliuawa na 13 kujeruhiwa.

Alisema mmoja wa watu waliouawa katika tukio hilo la ufyatuaji risasi alikuwa mtu anayehusishwa na tukio kama hilo lililotokea Saulsville mwaka jana.

“Hatuwezi kuondoa uwezekano kwamba matukio hayo yana uhusiano, na huenda yalikuwa ni shambulio la kulipiza kisasi,” alisema Mthombeni.