Mashabiki wa ndondi duniani sasa wanasubiri kutangazwa kwa tarehe rasmi ya pambano kati ya Anthony Joshua na Tyson Fury baada ya makubaliano ya awali kufikiwa.
Kwa sasa, pambano hilo linasubiri Joshua kumaliza kazi dhidi ya Kristian Prenga katika pambano lake la Julai nchini Saudi Arabia.
Iwapo Joshua atashinda, pambano dhidi ya Fury mwenye miaka 37 litakuwa mara ya kwanza kwa mabondia hao wawili wa Uingereza kukutana, licha ya wote kutawala kwa miaka mingi kwenye uzani wa juu duniani.
Pambano hilo linatarajiwa kuvutia mamilioni ya watazamaji duniani na kuingiza mapato makubwa, huku Saudi Arabia ikiendelea kujijenga kama kitovu cha mapambano makubwa ya ndondi kimataifa.
CHANZO: Newstimetr














