Mahakama Tanzania yafuta kesi iliyopinga ubunge wa Baba Levo

Baadhi ya malalamiko yaliyowasilishwa na wanachama wa chama cha upinzani ACT Wazalendo, ni pamoja na madai ya tuhuma za utekaji na rushwa.

Newstimehub

Newstimehub

16 Julai, 2026

4523619a beac 4bbb a8f8 484276c80c72 1784203477553 main

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma, Julai 16 imefuta kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa Mahakamani hapo na wananchi wanne (4) waliojitambulisha kuwa wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Mjini dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama tawala CCM Clayton Revocatus Chipando maarufu Baba Levo.

Uamuzi uliosomwa Mahakamani hapo na Jaji Victoria Nongwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo amesema hoja zote zilizoletwa na walalamikaji pamoja na ushahidi uliowasilishwa umekosa mashiko, hivyo kushindwa kuishawishi Mahakama kukubaliana nao.

Baadhi ya malalamiko yaliyowasilishwa na wanachama wa chama cha upinzani ACT Wazalendo, ni pamoja na madai ya tuhuma za utekaji na rushwa.