Kenya na DRC kurejesha uhusiano wa kidiplomasia

Mkutano huo uliandaliwa na Rais wa Congo Sassou Nguesso na Faure Essozimna Gnassingbe, kiongozi wa Togo.

Newstimehub

Newstimehub

23 Novemba, 2026

bc4ec535 21b5 4c8c a30a 068c2af63d2d 1795428283446

Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, zimekubaliana kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya miaka mingi ya mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yalifikiwa Novemba 22, 2026, wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi nne huko Oyo, Jamhuri ya Congo, uliohudhuriwa na Marais William Ruto na Felix Tshisekedi.

Mkutano huo uliandaliwa na Rais wa Congo Sassou Nguesso na Faure Essozimna Gnassingbé, kiongozi wa Togo.

Viongozi hao wawili walikubaliana kurejesha uhusiano wa kidiplomasia, kurejesha ushirikiano wa pande mbili, kuimarisha uhusiano wa kibiashara na usalama, na kushughulikia tofauti zitakazojitokeza katika siku zijazo kupitia mazungumzo ya kidiplomasia.

Mvutano wa kidiplomasia ulianza Disemba 2023 wakati (DRC) ilipoondoa ubalozi wake kutoka Kenya, kufuatia kuzinduliwa kwa muungano wa ‘Congo River Alliance’ (AFC) ambao unajumuisha kundi la waasi la M23.

Uhusiano huo uliendelea kuzorota mwaka 2025 baada ya Kenya kupendekeza kuteua wakilishi mkuu katika mji wa Goma—eneo linalodhibitiwa na M23—hatua ambayo ilipingwa na DRC.

Hatua hiyo ya upatanishi inatarajiwa kuboresha ushirikiano kati ya wanachama hao wawili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuimarisha jitihada za kikanda kushughulikia ukosefu wa usalama mashariki mwa DRC.