Idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya tetemeko la ardhi nchini Colombia, sasa imefikia 285.
Kulingana na Idara ya taifa ya majanga ya nchini humo (UNGRD), hadi kufikia sasa, watu 3,975 wamejeruhiwa na wengine 379 hawajulikani walipo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa UNGRD, shughuli za uokozi zitaendelea kupewa kipaumbele, hususani kwenye maeneo ambayo watu wanaaminika kuwa bado wamekwama kwenye vifusi.
“Kwa bahati mbaya, kuna uwezekano mdogo sana wa kuwapata watu ambao bado wako hai, japokuwa tutaendelea na mchakato wa kuwatafuta wale ambao bado hawajapatikana,” alisema Tamayo.
Agosti 10 mwaka huu, upande wa magharibi mwa nchi hiyo, ulikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richta 7.4, na kusababisha uharibifu mkubwa wa miondombinu muhimu.















