Mbali na kufanya mabadiliko katika Wizara ya Miundombinu, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye pia amefanya uteuzi mpya wa mawaziri wengine wawili katika kile kinachoonekana kama mini-reshuffle ya serikali.
Katika mabadiliko hayo, Fidele Nkezabahizi ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya ya Umma, huku Evelyne Butoyi akiteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari.
Nafasi ya Waziri wa Mawasiliano ilikuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa akihudumu katika nafasi hiyo, Gabby Bugaga, aliyefariki mapema mwezi huu baada ya kupatikana kwenye gari lililoharibika karibu na mji wa Bujumbura.
Wachambuzi wanaamini kuwa mabadiliko hayo yanaonyesha jitihada za serikali ya Burundi kuimarisha utendaji wake wa ndani wakati nchi ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kiuchumi na kijamii.
CHANZO: Newstimetr














