Ndege ya Jeshi la Anga la DRC yatangazwa ‘kupotea’

Ndege hiyo ya mizigo aina ya Cessna 208 ilikuwa inasafiri kutoka ene la Beni mkoa wa Kivu Kaskazini kuelekea Kalemie mkoa wa Tanganyika.

Newstimehub

Newstimehub

24 Novemba, 2026

ccbdedb3 5048 410a b913 88d9f13160b3 1795531097928

Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limepoteza mawasiliano na ndege yake ya mizigo kutokana na “hali mbaya ya hewa,” jeshi linasema siku moja baada ya waasi kudai kuwa wameiangusha ndege ya kivita ya serikali katika mapigano mashariki mwa nchi.

Ndege hiyo aina ya Cessna 208 ilikuwa ikisafiri kutoka eneo la Beni mkoa wa Kivu Kaskazini kuelekea Kalemie katika mkoa wa Tanganyika, msemaji wa jeshi Sylvain Ekenge alisema kwenye taarifa siku ya Jumatatu.

Kufikia siku ya Jumanne, ndege hiyo ilikuwa bado haijapatikana, na hatima ya waliokuwemo ndani haijulikani. Jeshi halijatoa taarifa zaidi kuhusu idadi ya waliokuwemo au sehemu ya mwisho ambapo ndege hiyo ilikuwepo.