Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na mwenzake wa Niger, Abdourahamane Tchiani, wamezungumza kwa njia ya simu kuhusu uhusiano wa nchi zao pamoja na masuala mbalimbali ya kikanda, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Jumatatu, Erdogan alisema kuwa juhudi na hatua za kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali zitaendelea, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki, NSosyal.
Aidha, Erdogan alisisitiza tena kuwa Uturuki inaunga mkono kikamilifu uhurua wa mipaka na usalama wa Niger. Alieleza pia utayari wa Uturuki kutoa msaada wote unaowezekana katika kuanzisha na kuimarisha michakato ya mazungumzo ya kikanda.
Vilevile, Erdogan alitoa salamu za rambirambi kwa Tchiani na wananchi wa Niger kufuatia kifo cha baba wa kiongozi huyo, kilichotokea wiki iliyopita.















