Mahakama Kuu ya Tanzania imemuondolea Tundu Lissu shtaka kuu la uhaini baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha viwango vya ushahidi vinavyohitajika kisheria kwa kosa hilo.
Hata hivyo, Mahakama hiyo imemtia hatiani Lissu kwa kosa dogo la uchochezi ndani ya shtaka hilo.
Shauri hilo, ambalo lilianza kusikilizwa majira ya saa tatu za asubuhi (kwa saa za Afrika Mashariki), linasikilizwa na jopo la majaji watatu wanaoongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.
Lissu alikuwa anakabiliwa na kesi ya uhaini tangu Aprili 2025 kufuatia kaunti na matamshi yanayohusiana na uchaguzi mkuu.















