Rais John Dramani Mahama siku ya Ijumaa alifanya ziara katika Hospitali ya Meli ya Mercy, yenye hospitali kubwa ya kiraia katika Bandari ya Tema, ambapo aliwashkuru kwa huduma zao maalum afya ambazo zimeleta mabadiliko makubwa kwa watu.
Wakati wa ziara hiyo, rais alijumuika na raia wa Ghana waliokuwa wanapata matibabu na kuwashkuru wahudumu na Waghana waliojitolea kwa ajili ya shughuli za miezi 10 za meli hiyo.
“Meli hizi zimekuwa zikitoa huduma kwa Ghana tangu 1991. Safari hizo zimesaidia kufanya upasuaji kwa watu zaidi ya 2,600 na kutibu watu 16,700 matatizo ya meno pamoja na kusaidia kuimarisha utaalamu wa wahudumu wa afya wa 139. Tunashkuru kwa huduma zao walizotoa kwetu,” alieleza.
Hospitali hiyo itakuwepo nchini humo kwa miezi 10 ikishirikiana na Serikali ya Ghana, ambapo watatoa huduma bila malipo ikiwemo kufanya upasuaji ndani ya meli.















