Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan arudishwa jela baada ya kutoka hospitali

Siku ya Jumanne, Mahakama Kuu ya nchi hiyo, iliamuru Khan, mwenye umri wa miaka 73, apelekwe katika hospitali binafsi ya Shifa iliyoko jijini Islamabadm kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya afya.

Newstimehub

Newstimehub

21 Agosti, 2026

b0debe2c ecf3 4ab4 af35 395995a730c1 1787306037390

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan amerudishwa tena gerezani siku ya Ijumaa, saa chache baada ya kutolewa hospitalini.

Siku ya Jumanne, Mahakama Kuu ya nchi hiyo, iliamuru Khan, mwenye umri wa miaka 73, apelekwe katika hospitali binafsi ya Shifa iliyoko jijini Islamabad kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya afya.

Khan, ambaye ni nyota wa zamani wa mchezo wa Kriketi nchini Pakistan, alipelekwa hospitalini kufuatia ombi lililotolewa na mawakili wake.

Khan, pamoja na mkewe, Bushra Bibi, wamepewa kifungo cha miaka 17 jela, katika kesi ambayo Khan mwenyewe, ameiita kuwa ya kisiasa.