Vikosi vya zimamoto nchini Hispania, vimefanikiwa kuokoa mifupa ya watu wanaosadikiwa kuwa ni watawala wa kale, kutoka kwenye monasteri moja nchini humo.
Uokoaji huo, umefanyika wakati wa eneo la monasteri hiyo, lilipokumbwa na moto nyika unaoendelea maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Moto nyika huo, ambao ulianza mwanzo wa wiki na kudumu hadi siku ya alhamisi, uliteketeza monasteri mbili za San Juan de la Pena, ambazo ni alama muhimu ya eneo la Aragon.
Moja ya monasteri hizo, inaaminika kuwa na kaburi la wafalme na watawala wa zamani wa kuanzia karne ya 10.
Idara ya dharura ya Hispania, ilionesha picha mjongeo za maofisa uokozi wakipambana kusalimisha mabaki hayo, yakiwemo mafuvu na mifupa ya watu hao.















