Iran: Hatuna mazungumzo yoyote na Marekani

Iran imekuwa na udhibiti wa njia hiyo toka kuanza kwa vita vya Mashariki ya Kati, Februari 28.

Newstimehub

Newstimehub

3 Agosti, 2026

688e8fd1 583e 45f3 aed6 96f2c3125bb6 1785750582160

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Esmaeil Baqaei  amesema kuwa taifa hilo halijafanya mazungumzo yoyote na Marekani kuhusu mustakabali wa Mlango Bahari wa Hormuz.

“Hatuna mazungumzo yoyote na Marekani, isipokuwa tuna mazungumzo na Oman kuhusu Oman kwa ajili ya Mlango Bahari wa Hormuz,” alisema waziri huyo.

Iran imekuwa na udhibiti wa njia hiyo toka kuanza kwa vita vya Mashariki ya Kati, Februari 28, mwaka huu.

Wakati huo huo, Iran imesisitiza kuwa njia hiyo itaendelea kurahisisha usafirishwaji wa nishati mbalimbali, kwa kupata kibali kutoka Iran.

Akizungumzia mazungumzo na Oman, Baqaei alisema kuwa, yanaridhisha, yakiwa na lengo la kuzindua njia mpya ya kupitia.

“Ni matumaini yetu kuwa, wenzetu watakubaliana na mpango huu,” alieleza.