Timu ya Wanapaleontolojia wamegundua aina mpya ya mjusi mkubwa nchini Zimbabwe, anayedhaniwa kuishi takribani miaka milioni 210 iliyopita.
Visukuku vya mjusi huyo, ambaye kitaalamu anafahamika kama, Musango matusadonaensis, vimegunduliwa katika katika fukwe za Ziwa Kariba, nchini Zimbabwe.
Visukuku vya mjusi huyo, vilianza kuchimbwa mwaka 2018.
Akiwa na urefu wa futi 15, kiumbe hicho kinaaminika kuwahi kuishi kipindi cha enzi za mijusi wakubwa.
Timu ya Wanapaleontolojia hao, ilihusisha wanasayansi kutoka Uingereza, Zimbabwe na Afrika.
Ugunduzi huo, umemuibua Mjusi wa Tendaguru, ambayo ni mabaki ya mjusi mkubwa aliyegundulika katika wilaya ya Lindi, Tanzania, ambaye alikuwa na urefu wa mita 43, akidhaniwa kuishi miaka milioni 150 iliyopita.
Sehemu kubwa ya mifupa yake ilichukuliwa na kupelekwa kwenye Museum für Naturkunde nchini Ujerumani, ambako imewekwa kama moja ya mifupa mikubwa zaidi ya dinosaria duniani.















