Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Sudan Kusini imetenga Disemba 22, 2026 kama siku ya kufanya Uchaguzi Mkuu nchini humo.
Kulingana na Mwenyekiti wa Tume ya NEC ya Sudan Kusini Abednego Akok Kacuol, siku hiyo inaenda sanjari na Sheria ya Uchaguzi wa nchi hiyo na mchakato wa upatikanaji wa amani ambao unafikia kikomo Disemba 2026.
“Uchaguzi utafanyika Disemba 22, 2026 kama ilivyoainishwa kwenye sheria ya uchaguzi,” alisema Akok katika mkutano wake na wanahabari siku ya Jumatatu.
Disemba 2024, serikali ya mpito ya umoja wa taifa, iliongeza muda wake kutoka Disemba 22, 2024, hadi Disemba 22, 2026.















