Rais wa Kenya William Ruto amemtunuku mwanariadha Sabastian Sawe zawadi maalum baada ya mafanikio yake ya kihistoria ya kuvunja rekodi ya dunia ya marathon.
Sawe amepokea gari aina ya Mercedes Benz S-Class pamoja na kiasi cha fedha kinachozidi dola za Marekani 60,000 kama sehemu ya kutambua mafanikio yake makubwa.
Mbali na zawadi za serikali ya Kenya, Sawe pia anatarajiwa kupata bonasi kubwa kutoka kwa waandaaji wa mashindano ya kimataifa na wadhamini kutokana na kuweka rekodi mpya ya dunia.
Mafanikio hayo yamezidi kuimarisha hadhi ya Kenya kama taifa kinara katika mbio za masafa marefu duniani.
CHANZO: Newstimetr














