Kwa mujibu wa msemaji wa MSS, Jack Ombaka, tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni likihusisha magari mawili ya aina ya MaxxPro, ambapo gari moja lilipokuwa likivuta jingine lilipata hitilafu ya kiufundi.
Maafisa waliojeruhiswa pamoja na raia walipelekwa katika Hospitali ya Lambert Santé iliyopo Pétion-Ville, ambapo afisa wa Kenya na raia mmoja walifariki dunia.
“Maafisa wa polisi wanane wa MSS walijeruhiwa, wanne wakiwa katika hali mbaya hivyo wanahitaji kuhamishwa kwa ajili ya kupata matibabu maalum nchini Jamhuri ya Dominika baada ya kupokea huduma ya kwaza katika Hospitali ya Aspen Level 2,” alisema Ombaka katika taarifa yake.
Aidha, Ombaka alitoa rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha baada ya tukio hilo.














