Venezuela yapanga kujiondoa ICC

Licha ya kujiondoa ICC, waendesha mashitaka wa mahakama hiyo, wamesisitiza kuwa, kesi za uhalifu wa kibinadamu zilizofunguliwa mwaka 2021, bado zitaendelea.

Newstimehub

Newstimehub

24 Julai, 2026

9a8a9fbf 2b80 4825 a9c8 e4394f30a0c4 1784923733260

Serikali ya Venezuela, imeujulisha Umoja wa Mataifa, nia yake ya kujiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Siku ya Ijumaa, serikali ya nchi hiyo ilimtumia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, taarifa rasmi za kujiondoa moja kwa moja kutoka ICC.

“Venezuela inaamini kuwa kuna upendeleo mkubwa wa kijiografia, ambao ni wazi kuwa umehamisha lengo zima la mahakama hiyo, huku ikizilenga zaidi nchi za Afrika na Marekani ya Kusini,” alisema Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Felix Plasencia.

Kulingana na Plasencia, hali hiyo inadhihirisha uminyaji wa haki na uonevu kwa nchi zingine.

Katka hatua nyingine, Plasencia aliituhumu ICC kwa kujiingiza ‘kwenye vita’ vyenye kulenga Wavenezuela kwa maslahi ya baadhi ya viongozi.

“Tutaunga mkono mifumo ya kisheria ambayo tu, inaheshimu utawala wa watu wengine,” aliongeza Plasencia.

Licha ya kujiondoa ICC, waendesha mashitaka wa mahakama hiyo, wamesisitiza kuwa, kesi za uhalifu wa kibinadamu zilizofunguliwa mwaka 2021, bado zitaendelea.