Mfalme wa Morocco amteua El Mansouri waziri mkuu wa kwanza mwanamke

Chama cha Fatima Ezzahra El Mansouri cha PAM kilishinda uchaguzi wa ubunge wa wiki iliopita na itabidi kiunde muungano na vyama vingine.

Newstimehub

Newstimehub

30 Septemba, 2026

9958d942 2820 43a0 9639 85844097e495 1790755942513

Mfalme wa Morocco amemteua meya wa mji wa Marrakesh Fatima Ezzahra El Mansouri kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo, baada ya chama chake kushinda uchaguzi wa ubunge wa wiki iliopita.

Chama chake cha mrengo wa kati cha PAM kilipata ushindi wa viti 97 kati ya 395 katika Baraza la Wawakilishi – ikiwa ni 31 zaidi ya chama kilichokuwa kwenye nafasi ya pili, licha ya kuwa idadi ya wapiga kura kwenye uchaguzi ilikuwa ndogo zaidi katika kipindi cha miongo miwili.

Baraza la Mfalme Mohammed VI sasa limempa jukumu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 50, ambaye pia ni Waziri wa Mipango na Makazi, “la kuunda serikali mpya”.

Kuunda muungano

Bila kuwa na wingi wa wabunge, chama cha PAM kitabidi kuunga muungano na vyama vingine kwa ajili ya muhula wake wa miaka mitano, pamoja na kuwa ufalme una mamlaka makubwa kuhusu sera muhimu nchini humo.

Chama cha PAM kiliasisiwa mwaka 2008 na mshauri wa sasa wa mfalme Fouad Ali El Himma.

El Mansouri pia alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa meya wa mji wa Marrakesh, akishinda uchaguzi 2009 kabla ya kupoteza nafasi hiyo miaka sita baadaye, kisha kurudi tena 2021.

Baraza la mawaziri la El Mansouri litabidi kukabiliana na masuala kadhaa ikiwemo ukosefu wa kazi na gharama za maisha, pamoja na tofauti zilizopo miongoni mwa watu hasa vijana.

“Vijana wanapitia changamoto na lazima tuwape suluhisho,” alisema wakati wa kampeni. “Tunataka turudishe matumaini, siyo tu kwa mazungumzo, lakini kwa suluhu thabiti.”

Uchaguzi wa bunge unakuja mmoja baada ya maandamano ya vijana ya Gen Z yaliyokuwa yanataka kuimarishwa kwa huduma za afya na elimu.