Kiwanda cha Dangote chabadili maamuzi kuhusu uuzwaji mafuta kwa sarafu ya Dola

Julai 14 mwaka huu, kiwanda hicho nchini Nigeria kilianza kuuza bidhaa zake za mafuta kwa Dola za Marekani katika soko la ndani, jambo ambalo limesababisha mjadala mkubwa.

Newstimehub

Newstimehub

24 Julai, 2026

98c5d9fd b7b6 47d0 a0ba 85c3c8592e5c 1784838508500

Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote nchini Nigeria kimebadili maamuzi yake ya awali, ya kuuza nishati ya mafuta, kwa kutumia Dola za Kimarekani.

Kampuni hiyo, imeweka bayana uamuzi huo, bila kutoa sababu za msingi, kupitia taarifa yake ya Alhamisi.

Julai 14 mwaka huu, kiwanda hicho nchini Nigeria kilianza kuuza bidhaa zake za mafuta kwa Dola za Marekani katika soko la ndani, jambo ambalo limesababisha mjadala mkubwa.

Kiwanda hicho kilisema kilifikia uamuzi huo kwa kuzingatia masuala mbalimbali, ikiwemo, ugumu wa kupata mafuta ya kutosha kupitia mpango wa serikali wa kununua kwa sarafu ya ndani ya Naira.

Sababu nyingine, ilikuwa ni kwa kuzingatia gharama za kimataifa, ambapo kampuni hiyo ilisema kuwa inanunua malighafi na kuendesha shughuli zake kwa kutumia dola, hivyo kuuza kwa dola kunasaidia kulinda biashara dhidi ya hasara.