Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori la Kenya (KWS) limeanza uchunguzi kufuatia vifo vya tembo 15 vilivyoripotiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini humo.
Vifo hivyo tata, vinadaiwa kutokea kati ya Juni 24 na Julai 24 mwaka huu.
Kulingana na KWS, wahifadhi wameanza kuchunguza mizoga ya wanyama hao ili kuweza kubaini vyanzo vya vifo vya tembo hao.
Wahifadhi hao wamebainisha kuwa, vifo vya baadhi ya wanyama hao, vilitokea nje ya eneo la hifadhi ambayo inapakana na Tanzania.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya KWS, Duncan Wanyama, amesema kuwa mizoga ya wanyama hao ilipatikana katika maeneo mbalimbali, nje ya mipaka ya hifadhi hiyo.
Kulingana na kanzi data ya Amboseli Trust for Elephants, eneo la Amboseli lilikuwa na zaidi ya tembo 2,000 elephants, ilipofika mwaka 2025.















