Wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema uamuzi wa Niger kufuta maandamano ya Mei Mosi ni ishara nyingine ya kuongezeka kwa hofu ya kiusalama katika ukanda wa Sahel.
Hatua hiyo imekuja wakati nchi jirani ya Mali nayo ikikabiliwa na mashambulizi makubwa ya makundi yenye silaha, jambo linaloongeza wasiwasi kuhusu usalama wa eneo zima la muungano wa AES unaojumuisha Niger, Mali na Burkina Faso.
Rais wa Niger Abdourahamane Tiani pia ametuma salamu za rambirambi kwa Mali kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni yaliyosababisha kifo cha Waziri wa Ulinzi wa Mali.
Wadadisi wanaona kuwa kufutwa kwa hafla za kitaifa kama Mei Mosi kunaonyesha ukubwa wa changamoto za kiusalama zinazolikumba eneo hilo.
CHANZO: Newstimetr














