Bunge lamtengenezea njia Rais wa DRC Tshisekedi kugombea muhula wa tatu

Bunge la Seneti limepitisha muswada wa kufanyika kwa kura za maoni ambao sasa utahitaji kuidhinishwa na Mahakama ya Katiba, alafu ifikishwe kwa Rais Felix Tshisekedi kwa ajili kutiwa saini.

Newstimehub

Newstimehub

17 Juni, 2026

56c1550d6dbb21226045c0faedc59e35cc98a6de0e5bd0cb14f2bf84800ee1f3

Bunge la Seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limepitisha miswada ya kufanyika kwa kura za maoni nchini humo, hatua itakayompa nafasi Rais Felix Tshisekedi kubadilisha katiba na kugombea muhula wa tatu.

Kura hiyo ya Seneti siku ya Jumatatu inakuja siku tatu baada ya maandamano ya waandamanaji wanaomuunga mkono na kumpinga Tshisekedi kukabiliana kuhusu mipango ya serikali ya kubadilisha katiba, ambayo upinzani inasema ni njia ya rais kutaka kuendelea kubaki madarakani.

Aliingia madarakani tangu 2019, Muhula wa pili wa Tshisekedi unafikia mwisho 2028.

Hata hivyo, rais huyo mwenye umri wa miaka 63 alisema mwezi uliopita kuwa atakubali kuendelea kuongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu “kama watu watataka” baada ya kura ya maoni kubadilisha katiba.

Ukomo wa mihula miwili

Muswada huo uliopitishwa na Bunge la Seneti, ambao uliidhinishwa na bunge la taifa mapema mwezi huu, ni wa utaratibu kuhusu kura za maoni.

Lakini unaweza kutengeneza njia ya kuondoa ukomo wa mihula miwili kwa marais, kulingana na katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.