Miss World akoshwa na mandhari ya Zanzibar, aimwagia sifa Tanzania

Molla ametembelea eneo hilo na kujionea urithi wa kihistoria na kiutamaduni unaolitambulisha kimataifa.

Newstimehub

Newstimehub

22 Novemba, 2026

72984df2 532d 4376 83ae f3f91fff66c1 1795352577465

Mlimbwende wa Dunia (Miss World 2026), Joheirry Molla, amekiri kuvutiwa na historia, utamaduni na mandhari ya kipekee ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Molla ametembelea eneo hilo na kujionea urithi wa kihistoria na kiutamaduni unaolitambulisha kimataifa.

Ziara hiyo ni sehemu ya safari yake nchini Tanzania pamoja na warembo wenzake kutoka mabara sita inayolenga kutangaza vivutio vya utalii, utamaduni na uzuri wa nchi kimataifa, kuelekea mashindano ya Miss World 2027 yanayotarajiwa kufanyika Tanzania.