Rais wa Cabo Verde, José Maria Neves, ameshinda muhula wa pili wa miaka mitano madarakani, kwa mujibu wa matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika Jumapili. Neves amewashinda wagombea wengine watano, akiwemo mwanamke wa kwanza kugombea urais nchini humo.
Kampeni za uchaguzi huo zilijikita zaidi katika umuhimu wa kuongeza fursa za ajira kwa vijana.
Matokeo yaliyotangazwa kupitia televisheni ya taifa, baada ya kuhesabiwa kwa kura katika asilimia 97 ya vituo vya kupigia kura, yalionyesha kuwa Neves alipata asilimia 63.8 ya kura, idadi iliyozidi asilimia 50 inayohitajika ili kuepuka kurudia kwa uchaguzi.
Matokeo yaliyotangazwa kupitia televisheni ya taifa, baada ya asilimia 97 ya vituo vya kupigia kura kuhesabiwa, yalionyesha kuwa Neves alipata asilimia 63.8 ya kura, idadi iliyozidi asilimia 50 inayohitajika ili kuepuka kurudiwa kwa uchaguzi.
Katika hotuba yake, Rosa alikubali kushindwa na kusema kuwa tayari alikuwa amempongeza Neves kwa ushindi wake.
Cabo Verde ni taifa la visiwa lililopo zaidi ya kilomita 600 magharibi mwa bara la Afrika. Nchi hiyo iliyokuwa koloni la Ureno ina takribani wakazi 500,000, ingawa idadi kubwa zaidi ya raia wake wanaishi nje ya nchi, wengi wao wakiishi Marekani na Ureno.
Cabo Verde ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye mifumo ya kidemokrasia iliyo imara zaidi. Hata hivyo, imekuwa ikipoteza vijana wengi wanaoondoka nchini humo kutafuta ajira katika mataifa ya nje.
Neves, mwenye umri wa miaka 66, aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka 15 kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais mwaka 2021. Anatoka katika chama cha zamani zaidi cha kisiasa nchini humo, Chama cha African Party for the Independence of Cabo Verde (PAICV), chenye msimamo wa kisiasa wa mrengo wa kati-kushoto.
Kwa upande wake, Rosa anatoka katika chama cha mrengo wa kati-kulia cha Movement for Democracy, ambacho kilikuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 10 kabla ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwezi Mei.
Cabo Verde inatumia mfumo mseto wa urais na ubunge. Katika mfumo huo, Waziri Mkuu ndiye anayeongoza shughuli za serikali, huku Rais akiwa na mamlaka muhimu, ikiwemo kura ya turufu ya kupinga au kurudisha sheria zilizopitishwa na bunge.















