Watu wasiopungua 25 waliuawa katika mashambulizi ya usiku katika kijiji kwenye jimbo la Plateau lililoko katikati mwa Nigeria, maafisa wa eneo hilo na wakazi walisema siku ya Jumanne, katika vurugu ambazo zimesababisha hali kuwa tete zaidi.
Msemaji wa polisi wa Plateau Alfred Alabo ameiambia Reuters kuwa maafisa walipelekwa eneo hilo na watatoa taarifa baada ya kutathmini hali.
Jamii katika jimbo la Plateau zimekabiliwa na vurugu katika siku zilizopita kati ya wakulima na wafugaji ambazo zinahusisha kulipiza kisasi, kusababisha vifo vya watu, na wengine kuondoka katika makazi yao.
Lemun Le’an Iliya, diwani anayewakilisha eneo hilo, anasema watu 23 waliuawa katika shambulio hilo na mwingine alifariki akiwa hospitalini.
Jimbo la Plateau, lililoko katikati mwa Nigeria, kwa muda mrefu limekumbwa na vurugu zinazohusishwa na migogoro ya ardhi, maeneo ya malisho na raslimali zingine, zikitatizwa zaidi na ukabila.















