Licha ya zuio kali lililotangazwa na Marekani, taarifa zinaonyesha kuwa baadhi ya meli bado zinaendelea kupita katika Mlango wa Hormuz, mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani.
Data za ufuatiliaji wa meli zinaonyesha kuwa takribani meli 15 zilipita katika mlango huo ndani ya saa 24, huku nyingine zikilazimika kubadili mkondo na kurudi nyuma kutokana na uwepo wa vikosi vya majini.
Miongoni mwa meli zilizopita ni za mafuta, gesi, kemikali pamoja na mizigo kutoka mataifa mbalimbali kama China, India na Brazil.
Hali hii inaonyesha kuwa licha ya hatua kali za Marekani, bado kuna mianya katika utekelezaji wa zuio hilo, jambo linaloongeza wasiwasi kuhusu mustakabali wa usalama wa nishati duniani.
CHANZO: Newstimetr














