Marekani pia inazingatia uwezekano wa kuzuia meli kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz kama sehemu ya mkakati dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya White House, Olivia Wales, hatua hiyo inalenga kupunguza mapato ya mafuta ya Iran ambayo yanachangia karibu nusu ya bajeti ya serikali.
Hata hivyo, wachambuzi wanaonya kuwa mpango huo una hatari kubwa, kwani unaweza kuchochea mashambulizi dhidi ya vikosi vya majini vya Marekani vilivyopo eneo hilo.
Mlango wa Hormuz ni njia muhimu ya kimataifa, ambapo takribani asilimia 20 ya mafuta duniani hupita kila siku.
CHANZO: Newstimetr











