Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Mlango Bahari wa Hormuz haujafungwa, lakini meli zinaogopa kupita kutokana na vita vinavyoendelea na Marekani pamoja na Israel.
Abbas Araghchi alisema kuwa tatizo kubwa ni hofu ya makampuni ya bima, ambayo yanakwepa kuhudumia meli kutokana na hatari ya vita.
Hata hivyo, Iran imeonya kuwa meli zinazohusishwa na mataifa yanayoshambulia zinaweza kushughulikiwa chini ya sheria za mzozo huo.
Hali hiyo tayari imeongeza gharama za usafirishaji na kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta duniani, huku uchumi wa kimataifa ukikumbwa na wasiwasi mkubwa.
CHANZO: Newstimetr













