Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana, amesema uwepo wa ATCL katika miji ya Johannesburg na Cape Town unachangia kukuza biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Mpango wa serikali kuongeza ndege unalenga pia kuimarisha mtandao wa safari za ndani na kimataifa, pamoja na kuchangia huduma za usafirishaji mizigo. Ongezeko la ndege hadi 24 ifikapo mwaka 2030 linatarajiwa kuongeza upatikanaji wa usafiri wa anga, kukuza uchumi, na kutoa huduma bora kwa abiria na biashara.
CHANZO: Newstimetr














