Shirika la Ethiopian Airlines limesema linafuatilia kwa karibu hali ya mgogoro Mashariki ya Kati, likionya kuwa linaweza kuongeza bei za tiketi iwapo hali haitaimarika.
Afisa Mkuu wa Biashara wa shirika hilo amesema kuwa ongezeko la bei ya mafuta kwa kati ya asilimia 16 hadi 17 linaweza kulazimisha hatua za haraka ili kulinda uendeshaji wa huduma.
Wakati huo huo, shirika hilo limepunguza safari katika baadhi ya miji ya Mashariki ya Kati kutokana na hali ya usalama na changamoto za kiuchumi.
CHANZO: Newstimetr














